JE, UNGEPENDA KUMPOKEA YESU KRISTO?

JE, UNGEPENDA KUMPOKEA YESU KRISTO? Would You Like to Receive Jesus Christ?

Labda unauliza, ” je, hii inatosha? Amka kwenda kazini, kupata pesa ili kuishi, fanya hivyo mara na mara.” kuishi kwa raha ya mda mfupi, lakini kwa maana duni?

Au pengine kiwwango chako cha kifo kinaendana nawe. Unahisi kuwa na hofu ya kifo, na kutokuwa na uhakika na kile kinachoweza kuwa zaidi ya hayo.

Labda mambo hayaendi ipasavyo. Maisha yamekuwa yasiyopangilika ” je, kuna njia nyingine nje ya hii treni inayoyumba? Unashangaa.

Ama labda umeboeka tu ” pointi inayonihusu mimi?”

Yesu anataka ujue kuna zaidi ya maisha kuliko yaliyopo sasa. Au kujifurahisha kwa raha na uzoefu wa aina mbalimbali. Au kuweka malengo na kuyatimiza.

Maisha HALISI yanapatikana kwako. Maisha yenye MAANA. Maisha yanayoleta furaha na utulivu SASA

Maisha yanayokuwezesha kuwa mtu muhimu na kukaa nyuma ya matokeo yenye maana.

Maisha yenye ahadi ya kupanuka zaidi ya kaburi hata katika kipimo kikubwa zaidi.

Yesu alisema, “nimekuja ili wawe na uzima na wawe nao tele tele” (yohana 10:10).

Maisha haya, maisha katika ufalme wa Mungu, yanapatikana kwako SASA.

Biblia inaita ” uzima wa milele,” si kwa sababu tu inaendelea milele, lakini kwa sababu ni uhai unaotoka katika umilele kuja sasa katika wakati uliopo.

Maisha haya ni muujiza wa kiungu katika roho ya mwanadamu ambayo huzaa imani, tumaini, na upendo.

Wale wanaolipokea hili “maisha kutoka juu” hufanyika wafuasi wa Yesu kristo na kuishi siku zao zilizosalia, si kwa ajili ya matakwa yao wenyewe, bali katika huduma ya Mungu.

Haya ni maisha yanayoishirikisha furaha, hata kama wewe ni maskini, au hauna kazi, au mlemavu, au kwa si maarufu, au upo gerezani, au bila familia.

Haya ni maisha ambayo pia huleta magumu ya kipekee. Ni bure kwa kuyaomba lakini itakugharimu kila kitu.

Vyovyote ulivyokuwa, vyovyote ulivyo, vyovyote unavyotumaini kufanya na kuwa. Kila kitu unachomiliki, HASWA mda wako na pesa, vitakuwa kwenye uangalizi wa Mungu.

Marafiki wa mda mrefu wanaweza kukukatia tamaa Familia yako mwenyewe inaweza kukukataa. Watu duniani kote leo wanaochagua kumfuata yesu kristo wanapoteza kazi, nyumba, mali, uhuru wa kusafiri, hata maisha yao kwa ajili ya Yesu.

Kwa kiwango kidogo zaidi, wengine wanaweza kukuona waajabu sana.

Kwa hivyo lazima uamue ” je, nitachagua kukubalika na ulimwengu – au nitachagua uzima katika Yesu kristo?”

Yesu alisema, ” je, itamfaa nini mtu akipata utajiri wote wa dunia na kuisahau nafsi yake?” (Mathayo 16:26)

Katika maisha yake, kifo, na ufufuo, Yesu kristo ameleta maisha HALISI – uzima kutoka chini ya utawala wa ibilisi na dhambi na mauti – na katika viwango vya sasa, ukweli wa kiungu unaojulikana kama ufalme wa Mungu.

Si tu utapata msamaha wa dhambi, lakini utapata uzima wa Mungu na uwezo ndani yako, unaobadilisha motisha yako ya ndani.

Upendo wa Mungu utaanza kupenya maishani mwako. Katika kupokea upendo wa Mungu, si tu utapata uponyaji kwa nafsi yako, utapata shibe kubwa zaidi inayodhihirika kwa wanadamu – kuishi ndani yake na kupanua upendo wa Mungu kwa wengine.

JE< UNGEPENDA KUWA MFUASI WA YESU KRISTO? Wewe fanya hivyo kwa kuweka tumaini lako katika Yesu.

Labda unaamini kuwa lazima ujiboresha kwanza kabla ya Kristo kukukubali. Huo ni uongo wa shetani Watu pekee ambao wanaweza kuja kwa Kristo ni wale ambao wanajijua wenyewe kuwa wenye dhambi.

Yesu alisema, ” sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi (luka 5:32).

Yesu anakukubali kama ulivyo Mabadiliko yatatokea, lakini baada ya Yesu kuingia katika maisha yako. Atakupa shauku mpya. Utajikuta unataka kufanya yaliyo sahihi na kuepukana na yale yaliyo maovu.

Ndiyo, itakuwa muhimu kwako kushikamana na matendo ya Mungu ndani yako na pamoja nawe. Hata hivyo, jambo la muhimu kwako kujua ni kwamba Yesu atafanya mabadiliko ya ndani huwezi kuyafanya mwenyewe.

Je, uko tayari kumpokea yesu kristo na kumfuata?

Bibilia inasema, “lakini kwa wale wote waliompokea, kwa wale walioamini kwa jina lake, aliwapa haki ya kuwa wana wa mungu” (yohana 1:12).

Yesu anakualika wewe mwenyewe kama ulivyo. Yeye anajua kila kitu kukuhusu. Mema, mabaya, na Ubaya – na anakukubali.

Amekusudia kukupa msamaha wake, ili kuingia maishani mwako kikamilifu, na kukufanya kiumbe kipya, kwa kadri unavyojifunza kumwamini na kumtii.

Bibilia inasema, “ukikiri kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka wafu, utaokoka. Maana kwa moyo unaamini hata kupata haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu” (warumi 10:9-10).

Je, unaamini katika Yesu? Kwa maneno mengine, je, unamwamini? Je, wewe ni tayari kujisalimisha kwake na kuwa mfuasi wake? Kama ni hivyo, maombi yafuatayo yanaweza kukusaidia.

” Bwana Yesu Kristo – nakuhitaji wewe. Nataka unichukue jukumu la maisha yangu Nasalimisha kila kitu changu kwako, Yaliyopita, ya sasa na yajayo. Naacha kujitawala mwenyewe – kuanzia sasa, Bwana, naomba uwe katika udhibiti.

Chochote unachopenda kufanya na maisha yangu tafadhali fanya Nakutaka zaidi ya kitu chochote. Nakupokea katika maisha yangu sasa hivi, Bwana yesu.

Bwana Mungu, nimekutenda dhambi, mimi mwenyewe, na wengine. Najuta na kutubu dhambi hizi. Nakataa kila dhambi kwa jina lake na ninaamini msaada wako wa kushinda kila moja (kiri na ikane kila moja kwa sauti mbele za Mungu).

Naamini ulipokufa msalabani, ulilipa adhabu ya dhambi zangu. Napokea msamaha wako sasa hivi Bwana Yesu, nashukuru nimesamehewa sasa. Asante Yesu!

Kwa sababu nimesamehewa sasa, Bwana Yesu, nachagua kusamehe kila mtu ambaye amewahi kutenda dhambi juu yangu. (kama majina yao yanakujia, tamka kwa sauti, ‘ kwa jina la Yesu Kristo, namsamehe (jina la mtu) na nimwache aende zake. ‘)

Bwana yesu kristo naomba sasa unibatize kwa Roho wako Mtakatifu. Nataka kujazwa na maisha yako na nguvu na kupokea kila zawadi ya kiroho unipayo. Nakutaka katika maisha yangu zaidi ya kitu chochote, Bwana Yesu.

Asante kwa kusikia maombi yangu na kujibu. Asante kwa kuja katika maisha yangu Sasa, Bwana, nifundishe kuishi maisha mapya. Ninakusudia kufuata wewe!

Nakupenda na nimejaa shukrani maana umeniokoa na kamwe hutaniacha wala hutanisahau. Ameeeeen.”

Je! mmejikabidhi kwa Yesu Kristo? Je, wewe sasa ni mfuasi wake? Kama hivyo, nakukaribisha katika familia ya Mungu!

Kila siku, chukua muda wako kuwa peke yake na Mungu, kuomba, kusikiliza mnong ‘ ono wa sauti ya Mungu ndani ya, na kusoma biblia.

Kama wewe si tayari kusoma biblia, mimi napendekeza kuanza na injili ya Yohana na kisha kusoma kwa hatua agano jipya.

Waambie wengine kwamba umempokea Yesu Kristo katika maisha yako.

Tafuta kanisa linalompenda Yesu, heshimu biblia, na kuwapenda watu wengine. Kuwa mshirika wa kawaida ya kusanyiko hilo!