KUMHESHIMU ROHO MTAKATIFU

KUMHESHIMU ROHO MTAKATIFU. Honoring the Holy Spirit.

Kama unakumbana na Mungu basi unakumbana na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni ” Mungu Duniani.”

Labda ndio maana Yesu alisema kwamba kila dhambi na kufuru za wanadamu zitasamehewa – isipokuwa kwa kukufuru (kumtibua kwa dharau) Roho Mtakatifu (angalia Mathayo 12:31).

Roho Mtakatifu ni Mungu. Kumkaribisha Roho Mtakatifu ni kumkaribisha Mungu. Kumzuia Roho Mtakatifu ni kumzuia Mungu. Kumhuzunisha Roho Mtakatifu ni kumhuzunisha Mungu. Kumheshimu Roho Mtakatifu ni kumheshimu Mungu.

Ni nini Mungu Roho Mtakatifu anafikiri kuwa ni heshima?

Kukiri kwa wazi wazi kuwa Yesu kristo ni Bwana.

1 wakorintho 12:3, Nataka mjue kwamba hakuna mtu anayezungumza na Roho wa Mungu kwa: ” Yesu alaaniwe,” na hakuna mtu awezaye kusema, ” Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu,” .

Kumwalika Roho Mtakatifu katika kila hali

Mithali 3:5-6: 3:5-6 Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitumaini akili zako mwenyewe; kwa njia zako zote mkiri, naye atatengeneza njia zako.

Kupokea nguvu za Roho Mtakatifu

1:8 Mtapokea nguvu Akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakua mashahidi wangu…

Kumsikiliza Roho Mtakatifu

Yohana 14:25-26 mambo haya nimewaambieni, nikiwa bado nanyi. Lakini huyo mshauri, Roho Mtakatifu, ambaye baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yale yote niliyowaambia.

Kujazwa na Roho Mtakatifu

Waefeso 5:18 usilewe kwa mvinyo, ambayo ndani yake mna ufisadi, Bali ujazwe Roho… roho…

Kukaribisha zawadi za Roho Mtakatifu

1 wakorintho 14:1 Ufuteni upendo, na kutaka sana karama za Rohoni, lakini zaidi mpate kuhutubu.

Hudumianeni kwa upendo

1 wakorintho 13:1 Nikinena kwa lugha ya wanadamu au ya malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

Kuimba kwa nyimbo za Roho kwa shukrani kwa Mungu.

Wakolosai 3:16 Neno la kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, nyimbo, na tenzi za rohoni, huku mkimwimbia Mungu kwa shukrani mioyoni mwenu.

Kutunza hatua na Roho

Wagalatia 5:16; 25 Basi nasema, enende kwa Roho, wala hamtatimiza kamwe tamaa za mwili i… kwa kuwa  tunaishi kwa Roho, tudumu pamoja na Roho.

Kuruhusu tunda la Roho kukua

Wagalatia 5:22-23 lakini tunda la Roho ni Upendo, Furaha, Amani, Uvumilivu, utu wema, , Uaminifu, upole na kiasi.

Kudumisha umoja wa Roho kupitia kifungo cha amani.

Wa Roho kwa kifungo cha amani.

Kuzungumza mmoja  na mwenziwe kwa kusaidiana, si kwa njia ya kumjeruhi,

Waefeso 4:29-31 Neno lolote ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo njema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.  Wala msimuhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya Ukombozi. Uchungu wote na ghazabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;