NI KIPI YESU ANACHOTOA?

NI KIPI YESU ANACHOTOA? What Jesus Offers.

Hili hapa ni historia yangu, Ingawa nililelewa katika kanisa la kikristo, simulizi kumuhusu Yesu katika Biblia zilionekana kama hadithi kwangu. Niliziheshimu, lakini zikuzichukulia kwa umakini. Kwa hakika hazikuweza kuwa na mguso katika maisha yangu.

Yaani nilikuwa na uhakika kuwa kama ungekuwemo ukweli wa kiroho ndani yake, basi ungehusu aina fulani ya mazingaombo ya watu wa Mashariki. Unaweza kufikiria mshuko wangu nilipokuta kutana kiroho na Mungu – Nikisikia kuhusu ufufuo wa Yesu! Nilishangazwa sana. Na Hata sasa.

Miongoni mwa mambo mengine, Yesus alinipa kujiheshimu. Sikufahamu ni kiasi gani nilikuwa mchafu, hadi nilipojisikia kutakaswa tena. Nilikuwa nikimuepuka Mungu. Sasa ninampenda Mungu. Roho Mtakatifu wa Yesu anaishi mwilini mwangu pamoja nami. Uwepo wake huo ndani yangu unanihakikishia kuwa ananipenda, kwamba ananisamehe dhambi zangu, na kwamba nitakwenda mbinguni nitakapokufa.

Yesu sasa ni jambo la muhimu sana katika maisha yangu. Najifunza jinsi ya kuishi kwa IMANI ndani yake.

Yesu ameniponya nafsi yangu. Amechukua maisha yangu na kuyafanya kuwa na manufaa. Kabla ya Yesu kuja katika maisha yangu, dhambi haikunisumbua – isipokuwa iliniingiza matatizoni. Sasa, Ninapogundua kuwa nimetenda dhambi, ninajisikia vibaya.

Kwa nini? Kwa sababu Yesu amebadili nia yangu ya ndani. Sitaki tena kutenda dhambi. Ninachokitaka ni kuwa mtiifu kwa Mungu Siyo kwa sababu atanitupa Jehanamu kama nisipomtii. Bali ni kwa sababu yeye anamaanisha kila kitu kwangu.

Kwa njia ya yesu, nimejifunza jinsi ya kutambua sauti ya Mungu kutoka ndani. Maisha kwangu sasa yamekuwa aina ya safari ya raha, kufuatia Neno lake la lililoandikwa na linalosemwa. Kila siku ni mwanzo mpya na Mungu. Ninapoanguka na kutenda dhambi, Yesu amenifunza haraka kurudi kwake, kupokea msamaha wake, kuchukua vipande, kuvibeba na kumfuata.

Je! Kitendo cha Yesu kuishi ndani yangu, kinanipa mimi kinga dhidi ya maumivu na shida? La hasha. Kiuhalisia, maumivu mengine na shida niliyoyapitia ni kwa sababu Ninamfuata Yesu. Lakini nimejifunza kwa msaada wangu mkuu kwamba Yesu kristo anashinda upinzani pamoja nami – na shida yangu yoyote kwa heshima yake mwenyewe.

NA WEWE JE?

Labda unajiuliza iwapo wewe ni mzuri kiasi! Kama ndivyo, unahitaji kuishi katika hofu kuhusu haki ya Mungu kwa ajili ya dhambi zako. Unaweza kuwekwa huru kutokana na mzigo wa mateso, “ Je nimefanya vya kutosha” Je maombi yangu yamekuwa bora? Je hadi mwisho Mungu atanirehemu?”

Yesu, kwa Roho wake, atauhakikishia moyo wako kuwa ndiyo, wewe sasa ni mwana au binti wa Mungu (si mtumwa), uliyekubalika kikamilifu katika macho yake kupitia dhabihu yake kwa ajili yako msalabani.

Yesu kristo alipokea haki uliyodaiwa na Mungu kwa ajili ya dhambi zako, zilizopita, za sasa na zijazo. Mungu ameifanya amani yake na wewe kwa njia ya Kristo. Unaweza kufanya amani yako na Mungu kwa kujiaminisha kwa Yesu Kristo na kumfuata yeye kama mwanafunzi wake.

Kutenda matendo mema ni muhimu sana. Kilicho muhimu ni nia iliyopo nyuma yake. Je matendo yako mema hutokana na upendo wa Mungu? Au ni kutokana na mtazamo wa hofu na Kufaidi?

Kwa njia ya Yesu, utagundua kwamba Mungu anakupenda kwa huruma, kama Baba anafurahi kwa mtoto wake. Zaidi ya hayo, ukifanya amani na Mungu kwa njia ya Yesu, Mungu hatabadilisha mawazo yake juu yako.

LABDA UNAISHI KWA HOFU YA ROHO WABAYA! Yesu Kristo anayo mamlaka kamili juu ya viumbe wote na nguvu za kiroho. Nimeona kwa macho yangu jinsi mapepo yaliwatoka watu yalipoamriwa kufanya hivyo kwa Jina la Yesu Kristo.

Labda unatafuta kuwekwa huru kutokana na matendo ya mwilii? Yesu anakupa njia isiyo na mwisho kwa ajili ya kuzaliwa kwako mara ya pili. Yesu atakusamehe dhambi zako sasa. Utakuwa na ufahamu ndani yako kwa Roho wa Yesu kuwa kuwa mwili wako unapokufa, moja kwa moja utahamishwa kwenye uwepo wake kamili, ukiwa umeponywa, na mwenye kujitegemea. Hautopotea kama mwanadamu wa kawaida.

Kama ulivyo ufufuo wa mwili wa Yesu, baada ya kifo, pia utapewa mwili wa ufufuo, mkamilifu, katika kila njia. Utapitia amani na furaha katika uwepo wake – NA – utajikuta unatumika sana katika p mbili, upendo wa Mungu na wanadamu wenzako. Biblia inafundisha kwamba badala ya kuharibiwa, utatawala na Yesu katika ulimwengu huu milele.

Kilicho zaidi, katika maisha haya, utapata kuongeza uhuru kutokana na “tamaa, chuki, na udanganyifu” kama wewe ukijifunza kwa uangalifu kukaa katika Roho wa Yesu Kristo. Yesu amekuja ili kwamba uweza kuanza maisha ya mbinguni sasa. “Raha -katika-uzima” inaweza kupatikana katika ushirika wa kila siku na Yesu Kristo.

Labda huna dini hata kidogo ila unauliza, ” maana ya maisha yangu ni nini? Je, maisha yangu yanathamani kwa jambo lolote?

Nataka mjue kwamba Yesu Kristo yu hai. Alifufuka kutoka kwa wafu na unaweza kukutana naye leo. Huwezi kumwona kimwili (pengine) lakini unaweza kukutana na Roho Wake. Na wewe utamtambua kuwa ni yesu

Yesu anautayari, kwa njia fulani, kukushika mkono ili aongoze maisha yako ya kila siku. Atakuongoza katika njia ambazo zitasababisha maisha yako kuwa na umuhimu wa kweli, sio tu harakati za kujifurahisha, wala tu kupambana kwa ajili ya kuishi. Zaidi ya hayo, atatumia maisha haya kama mafunzo kwa maisha yako yajayo.

Kila kitu unachokipitia sasa, Mungu atakitumia kwa mema ukitembea na Yesu.

Je, unamtaka Yesu Kristo maishani mwako?
Nilifanya video hii ya dakika saba ili kukusaidia kumpokea Yesu kama ungependa kufanya hivyo. Https://www.facebook.com/PastorScottHilborn/videos/1772161359493540/