USIOGOPE.

USIOGOPE. Do Not Be Afraid.

Yaweke moyo maneno haya ya ajabu ya Yesu Kristo:

Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwamini Mungu Niamini nami ” (Yohana 14:1).

Amani nawaachia; amani yangu nawapa. Sikupi kama dunia itoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu wala msiogope ” (Yohana 14:27).

Jipe moyo; ni mimi. Usiogope ” (Marko 6:50).

“Msiwaogope wale wauao mwili, lakini hawawezi kuuwa roho” (Mathayo 10:28).

Usiogope mambo yatakayo kupata ” (Ufunuo 2:10).

” Usiogope. Mimi ni wa Kwanza na wa Mwisho ” (Ufunuo 1:17)

JE, UNAKABILIWA NA MISUKO SUKO YA KUOGOFYA?

YESU angekwambia, JIKABIDHI KWANGU  WALA USIOGOPE.”

Ahadi ya Yesu SIYO kwamba utakwepa kuumia. Kuumia huja kwa kila mtu. Ukiungana na Yesu Kristo lakini hutapata MADHARA. Kuumia ni maumivu. Madhara ni uharibifu

Hata kama mabaya yatatokea, bado uko salama kwa Mungu. MAANGAMIZI hayatakuja kwako. Utavuka katika maisha haya yaliyoshikiliwa na Mungu.

Kwa aliye wa Yesu Kristo, haijalishi ni maumivu na mateso kiasi gani wanaweza kupitia, wanaweza kujua sasa kwamba YOTE YATAKUWA SAWA. 

UNGEPENDA KUJIKABIDHI KWA YESU KRISTO?

Kuyasalimisha mapenzi yako na maisha yako chini ya UANGALIZI  wa Mungu?

Kuweka uzito kamili wa UJASIRI wako kwake?

Kuanza kumtegemea?

KUMWAMINI Kwa yaliyopita, Yaliyopo sasa, na yale ya baadae?

KUPUMZIKA katika mamlaka na nguvu na utayari wake wa kukuokoa?

Ikiwa ni hivyo, maombi haya yanaweza kukusaidia kujikabidhi kwa Yesu. Ninapendekeza uiombe kwa sauti kubwa

” Bwana Yesu Kristo, nakuhitaji. Naamini ulikufa msalabani na ukafufuka kutoka kwa wafu kwa ajili yangu. Naamini unatawala sasa hivi juu ya ulimwengu huu.”

” Nirehemu, Bwana, na tafadhali unisamehe dhambi zangu nyingi. Naamini waweza kuniokoa na dhambi zangu na kunileta mbinguni nikifa. Kwa hivyo nakushukuru sasa kwamba umenisamehe.”

” Kwa ajili yako, Bwana Yesu, nami pia  nachagua kumsamehe yeyote aliyewahi kunikosea.”

” Bwana Yesu, naamini unaweza kuyatunza maisha yangu. Naamini umeishinda dhambi, mauti na shetani. Najikabidhi KWAKO Bwana Yesu.”

” Tafadhali njoo maishani mwangu, Bwana Yesu. Chukua mamlaka yako unitawale. Fanya upendavyo na maisha yangu. Ninasalimisha maisha yangu na mapenzi yako kutunzwa nawe, Bwana Yesu.”

” Unijaze Roho wako Mtakatifu, kwa nguvu zako za ajabu, kwa mtiririko wa pendo lako lisilokufa, na Kwa amani yako.”

” Ninaikataa hofu yangu sasa.”

” Nakupokea sasa hivi, Bwana Yesu.”

” Bwana Yesu wewe wajua ninayopitia maishani mwangu kwa sasa. UNAJUA mimi siwezi mwenyewe. Kwa hivyo nakukabidhi WEWE uyashughulikie. Nakuamini kwa kila kitu kinachonipa hofu, wasiwasi, au kukasirika.”

” Nionyeshe ni hatua gani ungetaka niichukue.”

Asante kwa kuja maishani mwangu, Bwana Yesu. Kwa jina lako lenye nguvu naomba Amina!”

Nakualika uende kwenye ukurasa wangu wa Facebook na tovuti yangu ambapo utapata makala na video zitakazokusaidia kukua katika uhusiano wako na Yesu Kristo.

https://www.facebook.com/PastorScottHilborn/