WASIFU MFUPI WA YESU.

WASIFU MFUPI WA YESU. Brief Biography of Jesus.
Yesu wa Nazareth alizaliwa takriban 6KK mjini Bethlehemu, mji wa kiyahudi katika jimbo la Yudea. Kama Wayahudi wote wa nyakati hizo, hakuwa na jina la Ukoo, lakini la Nazareti. Angejulikana kama Yesu mwana wa Yusufu, Seremala. Nje ya mji wake angetambulishwa kama Yesu wa Nazareth.

Yeye anaitwa Yesu Kristo na wafuasi wake, Kwa kuwa ” Kristo ” (Mpakwa Mafuta) ni neno la kigiriki kwa cheo cha wayahudi ” Masiyah.”

Kwa kitaalam, angeitwa Yesu Kristo lakini jina lake na cheo viliunganishwa mapema sana na wafuasi wake.

Yesu alizaliwa na Mariamu wa Nazareti, akapata mimba tumboni mwake kimuujiza kwa Roho Mtakatifu. Kuna uvumi katika injili ambao hata ukubwani, Wasiwasi ulibaki kuwa yeye ni haramu.
Yusufu, mume wa Mariamu, alikuwa mtu mwema na mcha Mungu, na inahisiwa alimfundisha Yesu shughuli yake, ambayo ilikuwa ya Useremala.

Nazareti inapatikana katika mkoa wa Galilaya, kaskazini mwa Israeli, siyo mbali na bahari ya Galilaya. Galilaya ilisadikika kuwa mahali pasipo na maendeleo. Wale wenye viwango vya juu waliishi mkoa wa kusini, Yudea.

Kwa Kuthaminisha, hapakuwa na wajajnja (wasomi wa dini) kutoka Galilaya, Kiasi kwamba watu walishangaa sana elimu na hekima ya Yesu wa Nazareti.

Mbali na kauli fupi zinazotumiwa kuwa Yesu alilelewa kama Myahudi, Mwaminifu kwa familia na jamii yake, hatupewi maelezo kuhusu maisha yake kutoka umri wa miaka 12 hadi 30.

Wale ambao baadaye walifanyika wafuasi wake hawataji chochote ambacho kingetusababisha Kuamini lolote zaidi ya kwamba Yesu aliishi Nazareti, alibeba taaluma yake kama seremala, na kwa uaminifu alitunza familia yake mara tu baada ya kifo cha baba yake Yusufu.

Yohana Mbatizaji, binamu wa Yesu, alitokeza kwa Waisraeli hadharani takriban Yesu alipotimiza Miaka 30. Yohana alitokea kujulikana zaidi kama Nabii wa Mungu. Aliwaita Wayahudi watubu dhambi zao na kubatizwa katika maandalizi ya ujio wa Masiyah na ufalme wa Mungu. Umati wa watu walimwendea Yohana kubatizwa naye katika mto wa Yordani.

Yesu pia alibatizwa na Yohana. Yesu alipopanda kutoka majini, Roho Mtakatifu alimjia kwa namna ya kuonekana, na sauti kutoka mbinguni ikasikika,

” Huyu ndiye Mwanangu, nimpendaye, ninayependezwa naye.” (mathayo 3:17)

Mara Yesu alivikwa nguvu za ajabu, akaanza kuponya wagonjwa, kutoa pepo, kuwasafisha wenye ukoma, kuwafufua wafu, na kuhubiri habari njema ya ufalme wa Mungu, hasa kwa maskini. Huduma yake ya mafundisho na kuhubiri iliendelea kwa miaka mitatu, kuanzia kule Galilaya. Japokuwa kwa wakati Katika Yudea na Samaria (mkoa ulio kati ya Galilaya na Yudea) Kadhalika Dekapoli, Nchi ya Wapagani mashariki mwa mto Yordani.

Ujumbe mkuu wa Yesu ulikuwa kwamba ufalme wa Mungu ulipatikana SASA kupitia kwake.

Katika miaka hii mitatu, akajikusanyia wafuasi wengi kwake, lakini kipekee kundi la ndani la watu kumi na wawili ambao baadaye angewaita ” Mitume.” Baada ya kufufuka kwake, Mitume hawa walikuwa mabalozi wa Yesu, walibeba mamlaka hiyo na nguvu za hali ya juu Kama alivyofanya yeye.

Yesu haraka akawa tishio kwa viongozi wa dini ya kiyahudi (walimu wa sheria na mafarisayo) kwa sababu ya umaarufu wake. Basi, wakafanya shauri juu yake na kumshawishi mmoja wa wanafunzi wake, Yuda iskarioti, ili kumsaliti.

Yesu aliwekwa kizuizini na Kayafa, Kuhani Mkuu wa kiyahudi, na kushtakiwa kwa kukufuru (akijidai kuwa Mwana wa Mungu). Alichukuliwa mbele ya mpokea kesi wa kirumi, pontio pilato, ambaye alikubaliana kuwa Yesu asulubiwe.

Baada ya kuchapwa bila huruma, Yesu alitolewa nje ya mji na kusulubiwa kati ya wezi wawili. Baada ya masaa machache Yesu alikata roho msalabani. Mwili wake uliwekwa katika kaburi la karibu, na kaburi lake likapigwa muhuri na kulindwa na askari. Hii ilifanyika Ijumaa (” ijumaa Kuu.”)

Siku ya Jumapili, siku ya tatu, Yesu alionekana hai kutoka mauti katika mwili usiokufa, na uliobadilishwa. Malaika waliondoa jiwe la kaburi ili wafuasi wake waone kuwa hakukuwemo tena.

Katika siku 40 zilizofuatia, Yesu aliwatokea wanafunzi wake mara nyingi, akiwatia moyo na kuwafundisha juu ya ufalme wa Mungu. Aliwatuma kwa maagizo haya:

” Nimepewa Mamlaka yote Mbinguni na Duniani. Basi, Enendeni mkawafanye Mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, mkiwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru. Na hakika nitakuwa pamoja nanyi hadi mwisho wa dahari.” (Mathayo 28:18-20)

Kisha Yesu akatoweka kutoka machoni pao, akapaa kwenda Mbinguni ambapo anatawala SASA juu ya vitu vyote duniani. Ameahidi kurudi kwa utukufu mwingi kuuhukumu ulimwengu na kufanya mambo yote kuwa sawa.

KWA KUHITIMISHA: Yesu ndiye vyote ujumbe NA Mwaliko wa biblia:

Mungu alikuwa akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake katika Kristo, bila kuhesabu dhambi za watu dhidi yao. Na hakika yeye ametupatia huduma ya upatanishi. Basi sisi ni Mabalozi wa Kristo, kana kwamba Mungu alikuwa akitoa rufaa yake kupitia sisi. Tunakusihi kwa niaba ya Kristo: upatanishwe na Mungu.” (2 wakorintho 5:19-20)

MUNGU AMEIFANYA AMANI YAKE NA WEWE KWA NJIA YA YESU.

Sasa lazima ufanye amani YAKO na Mungu.

Kwa jinsi gani?

Jiaminishe kwa Yesu Kristo, mpokee kama Mungu wako, na mfuate!